Jumatano, 18 Desemba 2013

WATU WAPATAO 200 WANUSURIKA AJARI YA NDEGE -ARUSHA TANZANIA

WATU WAPATAO 200 WANUSURIKA AJARI YA NDEGE -ARUSHA TANZANIA


Taswira ya picha eneo la tukuo
 
Habari iliyoifikia hivi punde toka jijini Arusha, inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha,hali iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo huku abiria zaidi ya 200 wakiwa ndani ya ndege hiyo mpaka sasa bila ya kushuka.

Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
Kwa habari zaidi usikose kutembelea  blog hii.
http://tanzanianewz.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni