Tanzania kuuza umeme nchi jirani.

Siku 7 tu baada ya shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutangaza kumalizika kwa mgao wa umeme wa siku kumi kwenye baadhi ya mikoa, Kaimu Mkurugenzi mtendaji Tanesco Felchesmi Mramba amethibitisha kwamba shirika lake linatarajia kufanya biashara ya kuuza umeme nje ya Tanzania.
Anakwambia ‘Uwezekano wa kuuza umeme nje ya nchi upo, tunatarajia mwaka 2016 ndio tutaanza kuuza manake kwa sasa ni kweli hatuna umeme wa kutosha kuuza ila mwaka 2015 ndio Tanzania itaanza kuzalisha umeme mwingi ambao ndio tutauuza 2016 baada ya kujenga transmission lines za kutuunganisha na majirani manake soko liko, Kenya na Zambia ni miongoni mwa nchi ambazo hazina umeme wa kutosha’
Bei ya umeme Tanzania iko chini sana ukilinganisha na majirani zetu, yetu ni senti 11.5 za Kimarekani, Uganda ni 17.5, Kenya ilikua 19 lakini juzi wameshusha na kuifanya 18.5 hivyo hata ukitulinganisha nao bado Tanzania tuko chini kwenye bei.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni