Jumanne, 7 Januari 2014

Kurasa za mwanzo na mwisho magazetini leo January 07 2014

Kurasa za mwanzo na mwisho magazetini leo January 07 2014

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Jumatatu, 6 Januari 2014

Majibu ya Mh Freeman Mbowe kuhusu tuhuma za Mh Zitto Kabwe

Majibu ya Mh Freeman Mbowe kuhusu tuhuma za Mh Zitto Kabwe

Mh Freeman Mbowe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alishusha tuhuma nzito dhidi ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, zikimhusisha na ufisadi.

Hata hivyo, Mbowe naye amejibu tuhuma hizo akisema ni busara zaidi kwa mhusika kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kuibua tuhuma nyingine.

Madai hayo ya Zitto kwa Mbowe ni kilele cha siasa za kuchafuana, kutukanana na kuvunjiana heshima kilichodumu kwa takribani miezi mitatu sasa kupitia vyombo tofauti vya habari.
Mimi nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu tuhuma hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine. Anapaswa kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.

“Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa
kwa malengo gani?

Yanga kwenda Uturuki Alhamisi

Yanga kwenda Uturuki Alhamisi

Wakati, Yanga wakipanga kuondoka nchini  Alhamisi kuelekea Uturuki, kiungo mchezeshaji wa timu  hiyo, Athuman Idd Chuji amekalia ‘kuti kavu’ endapo  atashindwa kuomba radhi kabla ya safari hiyo.
Kikosi Cha Yanga
Yanga imepanga kukaa wiki mbili nchini Uturuki huku ikiwa  na mipango ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki kujiandaa kwa ajili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Michuano  ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Kagame.

Katika safari hiyo, Yanga imeazimia kuondoka na  wachezaji wote isipokuwa Chuji ambaye amesimamishwa  kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu  ambao anadaiwa kuufanya wakati wa mechi ya  Nani Mtani  Jembe kwa kucheza chini ya kiwango na hata baada ya  kutolewa kuendelea kipindi cha pili, aliamua kuondoka  kabisa katika chumba cha kubadilishia nguo na kutokomea  zake.

Mtoto wa Sheikh Yahya Hussein atabiri mazitokwa Mwaka 2014.

Mtoto wa Sheikh Yahya atabiri mazito

Dar es Salaam. Mtoto wa aliyekuwa mtabiri bingwa, Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein ametabibiri kuwa Katiba Mpya itapatikana kwa mbinde, kwani kutakuwa na malumbano na utata hasa kuhusu ajenda ya Serikali tatu.
Maalim Hassan Hussein
Katika utabiri wake pia amesema kuna kiongozi mmoja wa chama cha siasa nchini ambaye atandolewa kwenye uongozi na kitendo hicho kinaweza kumsababishia anguko la kisiasa kwake au hata kifo.
Alisema hali kadhalika, kiongozi mmoja wa kisiasa mwenye wafuasi wengi na umaarufu mkubwa, mwishoni mwa mwaka huu ataugua kichaa na kumsababishia kuanguka kisiasa. Hussein alisema mbali na hayo, Tanzania itakumbwa na msiba wa kitaifa huku  umaarufu wa Rais Jakaya Kikwete, ukizidi kuongezeka hasa kwa kutatua migogoro mikubwa nchini.

Alisema Rais Kikwete pia atafanya tukio kubwa la kutikisa nchi, lakini tukio hilo litaleta neema.
“Uadui wa taasisi au chama utakuwa mkubwa na kuna dalili za kupigana kwa wafuasi wa vyama pinzani, Tanzania itaingia kwenye mzozo na nchi jirani na wanasiasa wataendelea kukumbwa na kashfa za ngono,” alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Maalim Hussein alisema, “Mwaka huu umenzia siku ya Jumatano na unaashiria shida, maradhi na vifo kwa watu maarufu wakiwemo wasanii na wanahabari.”

Alisema katika mambo ambayo ameyatabiri ni vyema Serikali ikawa makini kwani mwaka huu kuna majanga mengi ambayo yatatoke hasa vifo, shida na maradhi.

Alisisitiza kuwa kwa upande wanasiasa na viongozi wa dini watafariki, pia wasanii, wanahabari na wanasiasa. Hivyo ni vyema wakawa makini kwa mambo wanayoyafanya.

“Mwaka huu unaonyesha kuwa kutakuwa na neema kwa vijana hasa wasanii, wanahabari, lakini  kwa upande wa vifo inaonyesha watakufa wengi, ni vyema wakawa makini,” alisema  Maalim Hassan Hussein.

Kuhusu wanachama wa Chadema waliovuliwa uanachama leo

Kuhusu wanachama wa Chadema waliovuliwa uanachama leo

slaa
Leo Chadema wametangaza uamuzi yao juu ya wanachama wao Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kwa kuwavua rasmi  uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
mkumbo
Kamati Kuu ya Chadema ilikutana Januari 3-4, 2014 katika Ukumbi wa Mbezi Garden uliopo jijini Dar es Salaam,Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.
mwigamba
Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbroad Slaa amezungumza na wanahabari leo na kusema malengo ya waraka wa mabadiliko waliokutwa nao wahusika hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa viongozi wa chama.
Dr slaa pia ameongeza kwa kusema chama kinawatangazia wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh.Zitto Kabwe na washirika wake kwa jina la Chadema.
Source:Gpl

Picha mbalimbali katika Ajali ya Boti jana katika Bahari ya Hindi..

Picha mbalimbali katika Ajali ya Boti jana katika Bahari ya Hindi.

15
Taarifa inasema boti ya Kilimanjaro II iliyokua ikitokea Pemba kwenda Unguja January 5 2014 sehemu yake ya mbele ilizama kwa dakika kadhaa kwenye mkondo wa maji ndani ya eneo hatari la Nungwi ambapo watu kadhaa waliokua wamekaa sehemu hii ya mbele kwenye picha inayofuata hapa chini walibaki kwenye maji baada ya dhoruba hii.
Baada ya hapo inadaiwa ilibidi watu hao waachwe bila kuokolewa badala yake wakatupiwa vifaa vya kujiokoa na safari ikaendelea ili kuepusha boti nzima isizame.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia tanzanianewz.blogspot.com jana usiku (Jan 5 2013) zilisema katibu wa makamu wa pili wa Rais Znz akifanya mahojiano na Zanzibar cable TV alithibitisha kupatikana kwa maiti 5 na majeruhi watatu wakiwa taabani kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Unataka kuwa karibu na matukio mbalimbali yanayotokea nje na ndani ya Tanzania? ungana nami kupitia http://tanzanianewz.blogspot.com pia kupitia facebook fan page yangu https://www.facebook.com/photo.php?fbid=177650489096474&set=a.116953131832877.1073741825.116952488499608&type=1&source=11 tutakujuza zaidi.
14
1
Huyu ni miongoni mwa waliookolewa.
12
Hapa kwenye hii picha juu ni baada ya boti kuzama kwa sehemu ya mbele na kuibuka tena, ilipoendelea na safari abiria wote wakaamua kuvaa vifaa vya kujiokoa.
13
Kwenye picha ya juu na chini ni jinsi viti vilivyongo’lewa na maji yenye nguvu wakati sehemu hii ya mbele ilipozama kwa dakika kadhaa ambapo shuhuda Hamis alisema baada ya kuzama boti ilizima kwa dakika kama tano mpaka ikaanza kusogezwa na maji na kisha baadae ikakubali kuwaka ndio wakaendelea na safari.
16
17
18