Jumatatu, 6 Januari 2014

Majibu ya Mh Freeman Mbowe kuhusu tuhuma za Mh Zitto Kabwe

Majibu ya Mh Freeman Mbowe kuhusu tuhuma za Mh Zitto Kabwe

Mh Freeman Mbowe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alishusha tuhuma nzito dhidi ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, zikimhusisha na ufisadi.

Hata hivyo, Mbowe naye amejibu tuhuma hizo akisema ni busara zaidi kwa mhusika kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kuibua tuhuma nyingine.

Madai hayo ya Zitto kwa Mbowe ni kilele cha siasa za kuchafuana, kutukanana na kuvunjiana heshima kilichodumu kwa takribani miezi mitatu sasa kupitia vyombo tofauti vya habari.
Mimi nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu tuhuma hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine. Anapaswa kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.

“Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa
kwa malengo gani?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni