NDOA YAVUNJIKA RASMI WAVUTANA KURUDISHIANA FEDHA WALIZOPOKEA.
HABARI- kutoka nyumbani kwa familia ya Bi harusi ambayo ilikuwa
ikipinga ndoa isifungwe kutokana na Bwana harusi kushindwa kumalizia
sehemu ya Mahari zinadai kuwa ndoa imevunjwa rasmi na kilichobaki ni
mzozo wa kurudishiana fedha.
Pande hizo mbili ya Kiume na Kike zimengia kwenye Mzozo na kuvutana
kuhusu fedha baada ya Wazazi wa Mwanamke kukubali kurudisha fedha hizo
pamoja na vitu walivyopokea huku kikubwa kikiwa ni upande wa Mwanaume
kudai wapewe papo hapo.
Vitu vinavyodaiwa ni Fedha taslimu takribani Shilingi 310,000/=
ambazo zilitolewa kwa ajili ya Mkaja pamoja na kiingilio, Blanketi na
Mashuka.
Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao wako kila wakati unaokupa habari zisizoacha shaka kwa msomaji.
Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi |
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki |
Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akiwa anahuzunika na kushangaa wazazi wake kurudisha mahali ya mchumba wake |
–MBEYA YETU—
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni