Jumatatu, 6 Januari 2014

Yanga kwenda Uturuki Alhamisi

Yanga kwenda Uturuki Alhamisi

Wakati, Yanga wakipanga kuondoka nchini  Alhamisi kuelekea Uturuki, kiungo mchezeshaji wa timu  hiyo, Athuman Idd Chuji amekalia ‘kuti kavu’ endapo  atashindwa kuomba radhi kabla ya safari hiyo.
Kikosi Cha Yanga
Yanga imepanga kukaa wiki mbili nchini Uturuki huku ikiwa  na mipango ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki kujiandaa kwa ajili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Michuano  ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Kagame.

Katika safari hiyo, Yanga imeazimia kuondoka na  wachezaji wote isipokuwa Chuji ambaye amesimamishwa  kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu  ambao anadaiwa kuufanya wakati wa mechi ya  Nani Mtani  Jembe kwa kucheza chini ya kiwango na hata baada ya  kutolewa kuendelea kipindi cha pili, aliamua kuondoka  kabisa katika chumba cha kubadilishia nguo na kutokomea  zake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni