Jumamosi, 23 Novemba 2013

Huyu ndio anaetajwa kuwa mpenzi mpya wa D’Banj, aliwahi kuwa na Sean Kingston pia

Huyu ndio anaetajwa kuwa mpenzi mpya wa D’Banj, aliwahi kuwa na Sean Kingston pia.

db 6
Naona siku hizi habari nyingi ambazo mastaa hutaka ziwe siri, zinavuja kirahisi pale wanapokwenda kujirusha sehemu sehemu au wakati mwingine ushahidi watu wanautengenezea kutoka kwenye mitandao ya kijamii kama huu wa Instagram ambao ni maalum kwa kupost picha mbalimbali.
Baada ya utangulizi huo basi, naomba kukupa moja ya taarifa kubwa kwenye mitandao ya Nigeria kwamba mwimbaji D’Banj ameripotiwa kwamba yuko mapenzini na mrembo Yaris Sanchez raia wa Dominican Republic, nchi yenye watu zaidi ya milioni 10 kwa mujibu wa takwimu za WB 2012.
dbanj
Unaambiwa Mnigeria D’Banj na Yaris walichukua ndege private mpaka sehemu inaitwa Asaba huko Nigeria kwa ajili ya kwenda kula bata ambapo mrembo huyo aliamua kupost pichaz akiwa kwenye hizo bata za Nigeria.
db3
Mpaka sasa, mrembo huyu ambae ni mama wa mtoto mmoja ameshatajwa kwenye headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa dunia kama Fabolous, Sean Kingston, Lloyd Banks, Joe Budden na Bobby Valentino.
db8
Yaris na rapper Joe Budden wakati wa mapenzi yao..
db4
db2
db1
Hizi picha mbili za juu ni wakati Yaris alipokua Nigeria.
db 5

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni