BUNGE LAPINGA KUWEPO KWA DARAJA LA TANO KATIKA UFAULU WA WANAFUNZI KIDATO CHA NNE (DIV 5) http://Tanzanianewz.blogspot.com
Dar es Salaam.
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, imevikataa viwango vipya vya alama
za ufaulu kwa elimu ya sekondari vilivyotarajiwa kuanza kutumika mwaka
huu na kutaka utaratibu na alama zilizotumika mwaka jana, zitumike
kupanga matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa mwaka huu.
Serikali
ilitangaza utaratibu mpya wa alama za Mitihani ya Kidato cha Nne na
Sita kwa kufuta Daraja la Sifuri na kuleta Daraja la Tano.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stephen Ngonyani alisema jana kuwa kamati
hiyo ilichukua uamuzi huo kwa kuwa pamoja na udhaifu ulio kwenye alama
hizo, kamati yao haikuhusishwa katika mchakato wa kuandaa alama hizo.

Ngonyani
alisema waliagiza watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kuhakikisha wanaishirikisha kamati yao kwani imejaa walimu wanaoweza
kushauri vizuri.
“Hatutaki watuletee mambo ambayo yamewashinda baada ya kuyapeleka kwa wananchi,” alisema Ngonyani.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
akitangaza uamuzi huo mapema mwezi huu, alisema uamuzi wa kubadilisha
mfumo huo umechukuliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza mwaka
2012.
Alama
zilizokuwa zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),
katika kupanga matokeo hayo, kwa Kidato cha Nne ni A=80-100, B=65-79,
C=50-64, D=35-49, F 0-34 kwa upande wa Kidato cha Sita, A=80-100,
B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39.
Alama
mpya zilizotangazwa ni A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39,
E=20-29 na F=0-19. Alama hizo ni kwa kidato cha nne na sita.
Kwa
utaratibu huo, A ilitafsiriwa kuwa ni ufaulu uliojipambanua, B+ ni
ufaulu bora sana, B ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu,
E ufaulu hafifu sana na F ufaulu usioridhisha.
Katika
utaratibu huo, mtihani wa mwisho ulitarajiwa kuwa na alama 60 na alama
40 zitokane na alama za Maendeleo ya Mwanafunzi Shuleni (Continuous
Assessment-CA).
Mwaka
jana baada ya Serikali kufuta matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne,
Necta ilitumia CA ya 30 huku mtihani wa mwisho ukiwa na alama 70.
-MWANANCHI
Wadau
wa elimu na wabunge walipinga vikali utaratibu mpya wa alama za
mitihani hali iliyofanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuamuru wizara
husika kupeleka bungeni taarifa yenye maelezo juu ya uamuzi huo.
Kabla
ya Serikali kutoa kauli yake, watendaji na viongozi wa Wizara ya Elimu
walikutana na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii Mjini Dodoma mwezi
huu ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikataa viwango hivyo vipya na
kuitaka wizara kuendelea kuvifanyia kazi viwango hivyo kwa
kuishirikisha Bodi ya Necta.
Mjumbe
mmoja aliyekuwa ndani ya kikao hicho alisema hoja kuu zilizosababisha
kukataliwa kwa alama hizo ni ile iliyosemwa kuwa ni kushusha sana
viwango vya ufaulu, pia kutaka shughuli hiyo ifanywe kwa kushirikisha
Bodi ya Necta ambayo kisheria ndiyo yenye jukumu la kutunga sera za
mitihani.
“Tulichosema
ni kuwa viwango vya ufaulu pamoja na utaratibu uliotumika mwaka jana,
viendelee kutumika kwa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea kwa
sababu viwango vipya vimekosa uhalisia,” alisema mmoja wa wajumbe wa
kamati hiyo.
Wajumbe
hao walisema haiwezekani ufaulu wa A ukaanzia 75 wakati hakuna nchi
duniani yenye A ya namna hiyo, pia haiwezekani 20 ikahesabika pia kama
ufaulu.
“Pia
ukiangalia, Kifungu cha Nne cha Sura ya 10 ya Sheria ya Necta kinasema
kuwa taasisi hiyo ndiyo yenye jukumu la kutengeneza sera ya mitihani,”
alisema mjumbe huyo.
Hata
hivyo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
alisema bungeni kuwa daraja sifuri litaendelea kuwapo lakini
hakuzungumzia chochote kuhusu alama ambazo kamati ilishauri wizara hiyo
izifanyie kazi.
Mulugo
ambaye ndiye aliyehudhuria kikao hicho hakupatikana jana kuzungumzia
suala hilo. Hata alipopigiwa simu yake ya mkononi, iliita bila
kupokewa.
Ofisa
Habari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyanzu alisema
kwamba hana taarifa za maagizo hayo ya kamati hiyo.
Ufaulu wa chini
Kwa
mujibu wa kitabu kinachoonyesha viwango vya ufaulu duniani kila mwaka
cha International Qualification, baada ya Tanzania kutangaza alama hizo
mpya, sasa inaongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu.
Nchi
zinazofuatia kwa viwango vya chini baada ya Tanzania ni Kenya, Rwanda,
Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ambazo hata
hivyo, viwango vyake vipo juu kwa kiwango kikubwa vikilinganishwa na
vile vya Tanzania.
-MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni