Jumanne, 26 Novemba 2013

Habari za Vijana mwanzo wa Mahusiano na Mapenzi Mapenzi na Ujana hasaya Utotoni hatari sana!Tazama vijana wengi tunavyoweza kupoteza ndoto zetu kisa Kulazimisha mapenzi

 Habari za Vijana mwanzo wa Mahusiano na Mapenzi
Mapenzi na Ujana hasaya Utotoni  hatari  sana!Tazama vijana wengi tunavyoweza kupoteza ndoto zetu kisa Kulazimisha  mapenzi

 Tanzanianewz.blogspot.com




Mwanzoni sikumpenda kutoka
moyoni, nilimpenda kwa kuwa tyu
alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi
nilimtamani tu….yaani nilitegemewa
akinivulia nguo zake tukashiriki
tendo hamu yangu itaisha na
nitaachana naye.
Alinipenda sana, kadri siku
zilivyokwenda alizidisha upendo
wake kwangu.
Hakuna nilichohitaji kwake
akaninyima, aliwahi kumdanganya
baba yake kuwa anaumwa
akatumiwa pesa ilimradi anipatie
mimi nilipomwambia kuwa kuna
mtu ananidai.
Haikuwa kweli pesa ile niliitumia
kulipia chumba nikafanya uzinzi na
Fatuma.
Alihadithiwa habari hiyo, akalia kwa
uchungu mbele yangu, lakini neno
lake la mwisho likabaki kuwa
‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI
MWANAUME WA MAISHA
YANGU’……..Nilijisikia vibaya lakini
nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa
nilimkuwa katika mahusiano na
msichana yule kwa sababu moja tu…
NGONO…na katu hakutaka kushiriki
ngono na mimi. Alinikwepa sana
hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi
huenda ana mtu mwingine.
Msichana mrembo kama huyo
kamwe asingeweza kuishi bila
kufanya mapenzi. Hakika
haikuniingia akilini.
Nikaendelea na vimbwanga vya hapa
na pale.
Hakuchoka kunibembeleza,
hakuchoka kunipenda.
“Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa
nilikuwa nakupenda..” aliwahi
kunambia neno hilo. Japo lilinigusa
lakini sikulitilia maanani.
Hatimaye tukamaliza shule,
nikategemea kuwa ule muda wa
kumfaidi msichana yule kingono
ulikuwa umewadia.
Lakini haikuwa hivyo, akaendelea
kuwa mgumu huku akijitetea kwa
sabab u zisizokuwa na kichwa wala
miguu.
Sasa nikajikuta katika pepo mbaya,
nikaanza kumwonyesha hadharani
kuwa nina wanawake wengine. Japo
chozi lake liliniumiza sana lakini
sikujali.
Kwa nini ananinyima penzi binti
huyu? Nilijiuliza.
Hatimaye nikafikia uamuzi wa
kuachana naye.
Lakini siwezi kuachana naye bila
kumjua ladha yake.
Nikampangia shambulizi moja la
mwisho na kama ni ubaya uwe
ubaya tu.
Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa
mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai
hapa na pale nikamgusa matiti yake
madogo yaliyosimama wima
yakijitahidi kunidhihaki.
Nikamgusa huku na kule..nilipotaka
kumvua nguo akanizuia.
Nilikuwa nimelewa, nikaamua
kutumia nguvu, niliamua
KUMBAKA…..nikaichana sidiria yake,
kisha nikaiondoa chupi yake sasa
akabaki yu uchi wa mnyama.
Nikamrukia ili niweze kutimiza
lengo…
Kamwe sikuwahi kumwona binti
huyu akiwa katika uoga namna ile…
alikuwa amekodoa macho yake….na
alikuwa anatetemeka…
Akataka kukimbia uchi, nikamdaka
mkono.
Mara akatokwa na kelele kubwa sana
zilizonishtua sana.
Amakweli sikuzitegemea.
“ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI
ANANIBAAAKA…..”
Kelele zikawafikia wasamalia wema,
binti akaendelea kupiga kelele.
Hatimaye mlango ukavunjwa,
wasamaria wakanivagaa na kuanza
kunipiga……nilipigwa nikapoteza
fahamu.
Nilipozinduka nilijikuta na pingu
mkononi, pingu iliyounganishwa na
kitanda.
Nilikuwa na maumivu makali mwili
mzima. Nikakumbuka kuwa
nilifumaniwa nikitaka kufanya
ubakaji.
Baada ya kujitambua nilirejeshwa
mahabusu.
SIKU NNE baadaye nilikuja
kutolewa……hapakuwa na dhamana
lakini ilikuwa barua tu ya
kustaajabisha niliyokutana nayo.
“Mpenzi Christopher…..haikuwa nia
yangu kukusababishia kipigo kikali
na kuitwa mbakaji…nimefanya haya
kwa sababu nakupenda…napenda
uishi miaka mingi..Chriss ni wewe
mwanaume pekee niliyetokea
kuvutiwa naye kihisia…lakini nina
mapungufu makubwa…nina kasoro
kubwa…..Chriss mimi ningekuwa
muuaji iwapo ningekuruhusu
unibake….hivi chriss unadhani
mpapaso wako haukunisisimua?
Nilisisimka haswa na nilitamani
nikutimizie kwa hiari lakini
nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo
furaha na wala usisikitike kusikia
hili, mimi nimefurahi sana kufa
nikiupigania uhai wa mwanaume
niliyempenda, ninayempenda na
ninayekufa kwa ajili yake. Kitanzi
hiki kiwe kumbukumbu yako milele
kuwa NILIKUPENDA…….Chriss mimi
ni muathirika wa gonjwa la
UKIMWI…..laiti kama ungenibaka
basi leo hii ningekufa nikiwa
MUUAJI…ninafurahi kuwa nakufa
kama SHUJAA.”
Nilijikuta napoteza fahamu tena,
nilipozinduka nilikuwa nyumbani
kwetu…kila jicho lilinitazama kwa
namna yake……
AMA KWA HAKIKA nilikuwa na
mpenzi aliyenipenda kwa dhati…….
UPUMZIKE PEMA PEPONI…..kamwe
sitakusahau

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni