Jumanne, 7 Januari 2014
Jumatatu, 6 Januari 2014
Majibu ya Mh Freeman Mbowe kuhusu tuhuma za Mh Zitto Kabwe
Majibu ya Mh Freeman Mbowe kuhusu tuhuma za Mh Zitto Kabwe
Posted by Tanzanianewz
![]() |
Mh Freeman Mbowe |
MBUNGE wa Kigoma
Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alishusha tuhuma nzito dhidi ya
Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, zikimhusisha na ufisadi.
Hata hivyo, Mbowe naye amejibu tuhuma hizo akisema ni busara zaidi kwa mhusika kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kuibua tuhuma nyingine.
Madai hayo ya Zitto kwa Mbowe ni kilele cha siasa za kuchafuana, kutukanana na kuvunjiana heshima kilichodumu kwa takribani miezi mitatu sasa kupitia vyombo tofauti vya habari.
Hata hivyo, Mbowe naye amejibu tuhuma hizo akisema ni busara zaidi kwa mhusika kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kuibua tuhuma nyingine.
Madai hayo ya Zitto kwa Mbowe ni kilele cha siasa za kuchafuana, kutukanana na kuvunjiana heshima kilichodumu kwa takribani miezi mitatu sasa kupitia vyombo tofauti vya habari.
Mimi
nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu tuhuma
hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine. Anapaswa
kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.
“Mimi ni
mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama Freeman,
si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba
unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM
si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa
kwa malengo gani?
Yanga kwenda Uturuki Alhamisi
Yanga kwenda Uturuki Alhamisi
Posted by Tanzanianewz
Wakati, Yanga wakipanga kuondoka nchini Alhamisi kuelekea
Uturuki, kiungo mchezeshaji wa timu hiyo, Athuman Idd Chuji amekalia
‘kuti kavu’ endapo atashindwa kuomba radhi kabla ya safari hiyo.
![]() |
Kikosi Cha Yanga |
Yanga imepanga kukaa wiki mbili nchini Uturuki
huku ikiwa na mipango ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki kujiandaa kwa
ajili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Michuano ya Ligi ya Mabingwa
Afrika na Kombe la Kagame.
Katika safari hiyo, Yanga imeazimia kuondoka na
wachezaji wote isipokuwa Chuji ambaye amesimamishwa kwa muda
usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu ambao anadaiwa kuufanya
wakati wa mechi ya Nani Mtani Jembe kwa kucheza chini ya kiwango na
hata baada ya kutolewa kuendelea kipindi cha pili, aliamua kuondoka
kabisa katika chumba cha kubadilishia nguo na kutokomea zake.Mtoto wa Sheikh Yahya Hussein atabiri mazitokwa Mwaka 2014.
Mtoto wa Sheikh Yahya atabiri mazito
Posted by Tanzanianewz
Dar es Salaam. Mtoto wa aliyekuwa mtabiri
bingwa, Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein ametabibiri kuwa
Katiba Mpya itapatikana kwa mbinde, kwani kutakuwa na malumbano na utata
hasa kuhusu ajenda ya Serikali tatu.
![]() |
Maalim Hassan Hussein |
Katika utabiri wake pia amesema kuna kiongozi
mmoja wa chama cha siasa nchini ambaye atandolewa kwenye uongozi na
kitendo hicho kinaweza kumsababishia anguko la kisiasa kwake au hata
kifo.
Alisema hali kadhalika, kiongozi mmoja wa kisiasa
mwenye wafuasi wengi na umaarufu mkubwa, mwishoni mwa mwaka huu ataugua
kichaa na kumsababishia kuanguka kisiasa. Hussein alisema mbali na hayo,
Tanzania itakumbwa na msiba wa kitaifa huku umaarufu wa Rais Jakaya
Kikwete, ukizidi kuongezeka hasa kwa kutatua migogoro mikubwa nchini.
Alisema Rais Kikwete pia atafanya tukio kubwa la kutikisa nchi, lakini tukio hilo litaleta neema.
“Uadui wa taasisi au chama utakuwa mkubwa na kuna
dalili za kupigana kwa wafuasi wa vyama pinzani, Tanzania itaingia
kwenye mzozo na nchi jirani na wanasiasa wataendelea kukumbwa na kashfa
za ngono,” alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Maalim Hussein alisema, “Mwaka huu umenzia siku ya Jumatano na
unaashiria shida, maradhi na vifo kwa watu maarufu wakiwemo wasanii na
wanahabari.”
Alisema katika mambo ambayo ameyatabiri ni vyema
Serikali ikawa makini kwani mwaka huu kuna majanga mengi ambayo yatatoke
hasa vifo, shida na maradhi.
Alisisitiza kuwa kwa upande wanasiasa na viongozi
wa dini watafariki, pia wasanii, wanahabari na wanasiasa. Hivyo ni vyema
wakawa makini kwa mambo wanayoyafanya.
“Mwaka huu unaonyesha kuwa kutakuwa na neema kwa
vijana hasa wasanii, wanahabari, lakini kwa upande wa vifo inaonyesha
watakufa wengi, ni vyema wakawa makini,” alisema Maalim Hassan Hussein.Kuhusu wanachama wa Chadema waliovuliwa uanachama leo
Kuhusu wanachama wa Chadema waliovuliwa uanachama leo
Posted by: Tanzanianewz
January 5, 2014 General Newz

Leo Chadema wametangaza uamuzi yao juu ya wanachama wao Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kwa kuwavua rasmi uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

Kamati Kuu ya Chadema ilikutana Januari 3-4, 2014 katika Ukumbi wa Mbezi Garden uliopo jijini Dar es Salaam,Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbroad Slaa amezungumza na wanahabari leo na kusema malengo ya waraka wa mabadiliko waliokutwa nao wahusika hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa viongozi wa chama.
Dr slaa pia ameongeza kwa kusema chama kinawatangazia wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh.Zitto Kabwe na washirika wake kwa jina la Chadema.
Source:Gpl
Picha mbalimbali katika Ajali ya Boti jana katika Bahari ya Hindi..
Picha mbalimbali katika Ajali ya Boti jana katika Bahari ya Hindi.

Taarifa inasema boti ya Kilimanjaro II iliyokua ikitokea Pemba kwenda Unguja January 5 2014 sehemu yake ya mbele ilizama kwa dakika kadhaa kwenye mkondo wa maji ndani ya eneo hatari la Nungwi ambapo watu kadhaa waliokua wamekaa sehemu hii ya mbele kwenye picha inayofuata hapa chini walibaki kwenye maji baada ya dhoruba hii.
Baada ya hapo inadaiwa ilibidi watu hao waachwe bila kuokolewa badala yake wakatupiwa vifaa vya kujiokoa na safari ikaendelea ili kuepusha boti nzima isizame.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia tanzanianewz.blogspot.com jana usiku (Jan 5 2013) zilisema katibu wa makamu wa pili wa Rais Znz akifanya mahojiano na Zanzibar cable TV alithibitisha kupatikana kwa maiti 5 na majeruhi watatu wakiwa taabani kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Unataka kuwa karibu na matukio mbalimbali yanayotokea nje na ndani ya Tanzania? ungana nami kupitia http://tanzanianewz.blogspot.com pia kupitia facebook fan page yangu https://www.facebook.com/photo.php?fbid=177650489096474&set=a.116953131832877.1073741825.116952488499608&type=1&source=11 tutakujuza zaidi.


Huyu ni miongoni mwa waliookolewa.

Hapa kwenye hii picha juu ni baada ya boti kuzama kwa sehemu ya mbele na kuibuka tena, ilipoendelea na safari abiria wote wakaamua kuvaa vifaa vya kujiokoa.

Kwenye picha ya juu na chini ni jinsi viti vilivyongo’lewa na maji yenye nguvu wakati sehemu hii ya mbele ilipozama kwa dakika kadhaa ambapo shuhuda Hamis alisema baada ya kuzama boti ilizima kwa dakika kama tano mpaka ikaanza kusogezwa na maji na kisha baadae ikakubali kuwaka ndio wakaendelea na safari.



Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)