Jumatano, 30 Oktoba 2013
http://tanzanianewz.blogspot.com
MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU:
UMUHIMU WA KUJITAMBUA KUPITIA TABIA YA MUNGU
Ni jambo muhimu sana kwa kijana yeyote anayetaka kuoa au kuolewa kujua tabia ya Mungu kabla hajafikia uamuzi wa kuoa. Hii itamsaidia kujitambua yeye ni nani na kutengeneza mahusiano bora zaidi na Mkewe. Ieleweke kwamba Mwanadamu aliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, hivyo ni dhahiri kwamba hatua ya kwanza mtu anayopaswa kuchukua katika kutafuta kujitambua ni kutafuta kumjua Mungu na tabia yake. Imeandikwa katika Ayubu 22:21
“Mjue sana Mungu ili uwe na amani, ndivyo mema yatakavyokujia.”
Kumjua Mungu ndiko kunakompelekea mtu kujitambua yeye ni nani. Njia pekee ya kumjua Mungu ni kwa kutafuta kujua tabia ya Mungu kupitia kazi zake. Mtume Paulo anaandika katika Warumi 1:20 akisema;
“Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani uweza wake wa milele na Uungu wake;…”
Mungu aliazimia tangu mwanzo kuonekana kwa wanadamu, namna pekee aliyotengeza ili tupate kumwona ni kupitia kazi zake. Tunapata kumjua Mungu kupitia kazi zake alizozifanya, anazozifanya na atakazoendelea kuzifanya kupitia wanadamu na katikati ya wanadamu.
Biblia inaweka wazi kuwa Mungu ndiye msanifu wa Ndoa na ndiye atoaye mke mwema na mwenye busara. Kutambua tabia ya Mungu kunamsaidia kijana kuwa na mtazamo sahihi juu ya mke aliyepewa na BWANA na Ndoa kwa ujumla. Ni dhahiri kwamba ikiwa Mungu ndiye atoaye mke mwema, basi mke huyu ni kitu chema kama Mungu alivyomkusudia.
Ni Muhimu kutambua kwamba kazi ya mtu yeyote, ndani yake hubeba tabia ya mhusika; kwa kuwa mtazamo na tabia ya ndani ya mtu (internal attitude and character) ndiyo inayoweka msingi wa namna mtu anavyoatafsiri mambo mbali mbali katika maisha yake ya kila siku. Ni kwa jinsi hii ambapo hata kazi azifanyazo mtu ni matokeo ya namna anavyoutazama na kuutafsiri umuhimu wa kazi hiyo, namna ya kuifanya na mambo mengine yanayohusiana na kazi husika.
Mwanadamu aliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Hivyo ni dhahiri kwamba tabia njema ya mwanadamu ina asili yake toka ndani ya Mungu aliye asili ya vitu vyote. Biblia inaweka wazi katika Nehemiah 6:9 kwamba;
“Mbingu, na mbingu zake pamoja na jeshi lote la nchi ni kazi ya mikono ya Mungu”
Imeandikwa pia na mtume Paulo katika Waefeso 2:10 kwamba;
“…tu kazi ya mikono yake, tuliumbwa na Mungu katika Kristo Yesu tutende matendo mema ambayo tangu awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo”
BWANA Yesu katika Yohana14:12 anasema;
“…yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo atazifanya, naam na kubwa kuliko hizo atafanya, maana mimi nakwenda kwa baba.”
Mambo ya msingi ambayo tungependa uyaone katika mistari hii ni kwamba;
MWANADAMU NI MFANO HALISI WA MUNGU
Hii inatusaidia kutambua kwamba tabia ya mwanadamu katika utendaji kazi lazima ifanane na Mungu. Tunaweza kutambua tabia ya Mungu katika utendaji kazi kwa kutazama kazi njema zinazofanywa na wanadamu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu (Watu waliookoka, wanaoongozwa na Roho wa Mungu). Mtu yeyote aliye okoka ndani yake amerejeshewa mfano halisi wa Mungu, na ana uongozi wa roho Mtakatifu anayemsukuma kutenda sawa na mapenzi ya Mungu wakati wote. Hivyo matendo yake ni lazima yaidhihirishe na yathibitishe tabia ya Mungu
MATENDO MEMA YALISHAANDALIWA NA MUNGU
Yapo matendo mema ambayo Mungu alishayaandaa tangu kabla ya kuweka misingi ya ulimwengu ili wanadamu wapate kuenenda nayo. Mwanadamu yeyote anayeenenda katika matendo hayo anadhihirisha na kuithibitisha tabia ya Mungu katika utendaji wake kwa kuwa matendo haya ndani yake yamebeba fikra na kusudi la Mungu kwa maisha ya Mwanadamu.
UWEZO WA KUZITENDA KAZI ZA MUNGU
Kwa njia ya imani katika Kristo Yesu (Wokovu) tumepewa uwezo wa kutenda na kuzidhihirisha kazi za Mungu, naam kazi kubwa zaidi ya zile zilizofanywa na BWANA Yesu alipokuwa duniani. Tunapodhihirisha na kutenda kazi hizi ndani yake tunadhihirisha tabia ya Mungu na hivyo kuwezesha watu kumwona na kumjua Mungu.
Ndani ya kazi tuzifanyazo kuna tabia yetu ambayo huandikwa ndani ya hizo kazi; kadhalika Mtu anapokuwa na tabia ya Kristo (Tunda la Roho), Matendo yake na kazi zake zinadhihirisha tabia ya Kristo. Ili kujua tabia ya Mungu ni muhimu sana kujua na kuzitazama kazi azifanyazo kupitia wanadamu, ndani ya wanadamu, na katikati ya wanadamu. Hizo zinaweza kufunua siri kubwa sana kuhusu tabia ya Mungu.
Tunaweza kujifunza mambo mengi kuhusu tabia ya Mungu kwa kuziangalia kazi alizozifanya, azifanyazo, na atakazoendelea kuzifanya katikati ya wanadamu. Kazi hizi huweza kuleta ufunuo wa tofauti kabisa juu ya Mungu na tabia yake halisi.
Baadhi ya mambo ya tuliyojifunza kuhusiana na tabia ya Mungu ambayo ni ya msingi hasa mtu anapotaka kufanya uamuzi sahihi wa kuoa ni kama ifuatavyo;
MUNGU NI MKAMILIFU NA NI MUNGU WA UKAMILIFU.
Tabia hii ya Mungu inadhihirika wazi katika kazi yake ya uumbaji kama inavyoelezwa katika kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza na ya pili. Hakuna kazi hata moja ambayo Mungu aliianza kisha akaiachia njiani, kila siku Mungu alihakikisha amekamilisha kile alichokusudia kukifanya na kuhakikisha kimekuwa kamili, kinapendeza na akakifurahia.
MUNGU NI WA MILELE NA NI WA UMILELE
Nabii isaya katika Isaya 9:6 anataja jina lake kuwa ni “Baba wa Milele” kadhalika kazi yeyote aifanyayo Mungu hubeba asili hii ya Mungu. Mhubiri 3:14, anaweka wazi kabisa kwamba;
“Kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele, hakuna awezaye kuipunguza kitu wala kuizidisha kitu, na hii Mungu amefanya ili watu wamche yeye.”
Ni dhahiri basi kitu chochote chenye asili ya Mungu hudumu na wala hakiwezi kuishia njiani kwa kuwa kama jinsi yeye aliyekianzisha alivyo wa Milele ndivyo kazi yake ilivyo, ili kumletea utukufu Mungu aliye hai.
MUNGU NI MTAKATIFU NA NI MUNGU WA UTAKATIFU.
Neno “Mtakatifu” ni jumla ya asili na tabia ya Mungu jinsi alivyo, hii ndiyo sababu wale malaika waliopo katika kiti cha enzi cha Mungu wanaomwabudu Mungu huitana kila mmoja na mwenzake wakisema “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu” (Isaya 6:3, Ufunuo 4:8) kwa kuwa neno hili ni jumla ya asili ya Mungu na tabia yake jinsi ilivyo. Imeandikwa katika 1Petro1:15.
‘…Bali kama yeye aliyewaita alivyo Mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.
Tena imeandikwa katika 1Petro 1:16 kwamba
“Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.”
Biblia inaweka wazi kabisa katika Waefeso 1:4 kwamba Mungu alituchagua tangu kabla ya kuweka misingi ya ulimwengu ili tuwe “watakatifu” yaani watu wenye kufanana na yeye katika jumla ya asili na tabia yake.
MUNGU NI UPENDO NA NI MUNGU WA UPENDO
Imeandikwa Mungu ni upendo , na ndani yake hakuna chuki. Tabia hii ya Mungu pia inadhihirika katika kazi za Mungu kwa mfano mpango wa wokovu. Imeandikwa katika Yohana 3:16;
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu; hata akamtoa mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”
Tena imeandikwa katika waraka wa kwanza wa Yohana 4:16;
“Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake”
Mwanadamu yeyote aliye ndani ya Kristo na Kristo akiwa ndani yake, anao uwezo wa kuzihirisha nguvu ya upendo wa Mungu katika kazi azifanyazo.
MUNGU NI WA AMANI WALA SI WA MACHAFUKO
Mtume Paulo meweka wazi kabisa tabia hii ya Mungu katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho 14:33. Nabii isaya pia katika Isaya 9:6 alimshuhudia BWANA Yesu kuwa jina lake ni “Mfalme wa Amani.” Ufalme wa Mungu pia umetafsiriwa na mtume Paulo kuwa ni Haki, Amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Warumi 14:17) Ni dhahiri basi kitu chochote chenye asili ya Mungu kimebeba tabia hii ya Mungu. Huleta amani, utulivu na ustawi.
MUNGU NI MWAMINIFU NA NI MUNGU WA UAMINIFU
Mungu hawezi kusema uongo wala hawezi kujuta. Imeandikwa katika Hesabu 23:19;
Mungu si mtu hata aseme uongo; wala si mwanadamu, ajute; iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Mtume Paulo ameandika pia habari ya uaminifu wa Mungu katika Warumi 3:3-4, akisisitiza kutokuamini kwetu hakubatili uaminifu wa Mungu. Mtu yeyote aliye okoka mwenye Roho wa Mungu anayemuongoza toka ndani yake huthibitisha tabia hii ya uaminifu. Ni kwa kumtazama mtu wa jinsi hii tunaweza kujifunza juu ya uaminifu wa Mungu kwa kuwa ndani yake amerejeshewa mfano halisi wa Mungu.
Yapo mambo mengi ambayo tungeweza kuyaainisha kama sehemu ya tabia ya Mungu, kwa sababu hiyo tunapenda kukushauri utumie muda wako kujifunza na kujaribu kumtafakari Mungu kwa macho ya kutaka kujua tabia yake. Hii itakusaidia kujua tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya shetani hivyo kuchukua hatua sahihi katika maisha yako.
UFAHAMU JUU YA NDOA

Jumatatu, 28 Oktoba 2013
Jumapili, 27 Oktoba 2013
Sammisago.com: Pole Kwa Familia Ya Wema Sepetu Kwa Kumpoteza Baba...
Sammisago.com: Pole Kwa Familia Ya Wema Sepetu Kwa Kumpoteza Baba...: Kupitia sammisago.com tunawapa taarifa zilizotufikia kuwa Miss Tanzania 2006, Wema .A. Sepetu Amefiwa na Baba yake mzazi, Balozi Isaac ...
Ijumaa, 25 Oktoba 2013
Jumatano, 23 Oktoba 2013
MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 23/10/2013 YA MICHEZO | TANZANIA NEWZ
MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 23/10/2013 YA MICHEZO http://tanzanianewz.blogspot.com
Jumanne, 22 Oktoba 2013
MASAI NYOTAMBOFU: AJALI YA KUTISHA MKOANI MBEYA: CHEKI GARI AINA YA ...
MASAI NYOTAMBOFU: AJALI YA KUTISHA MKOANI MBEYA: CHEKI GARI AINA YA ...: GARI AINA YA SUZUKI NA NISSAN ZIMEGONGANA USO KWA USO MAENEO YA IWAMBI JIJINI MBEYA MCHANA WA LEO KISA CHA
Mafundisho Ya Neno la Mungu: SOLOMON MKUBWA: Nilipoteza Mkono Wangu Baada Ya Ku...
Mafundisho Ya Neno la Mungu: SOLOMON MKUBWA: Nilipoteza Mkono Wangu Baada Ya Ku...: “Nikiwa na miaka 12, nilipata matatizo ya uvimbe kwa mkono wangu wa kushoto. Uvimbe huo ulikuwa wa ajabu sana na hakuna aliyefahamu chanzo...
Mafundisho Ya Neno la Mungu: WAJIBU WA WAZAZI KWA VIJANA NA WATOTO
SOMA NA PATA ELIMU JUU YA MAISHA YA NDOA NA UWEPO WA MUNGU KATIKA MAHUSIANO YA NDOA
Mafundisho Ya Neno la Mungu: WAJIBU WA WAZAZI KWA VIJANA NA WATOTO: UJUMBE UNATOKA: Kumb la torati 6:6-7 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wak...
Jumamosi, 19 Oktoba 2013
Ijumaa, 11 Oktoba 2013
Alhamisi, 10 Oktoba 2013
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)