Jumatano, 27 Novemba 2013

Stori kuhusu hili gari linalojiendesha lenyewe, limefanyiwa majaribio Japan… Video na na Picha.


Stori kuhusu hili gari linalojiendesha lenyewe, limefanyiwa majaribio Japan… pichaz na video.



Stori kuhusu hili gari linalojiendesha lenyewe, limefanyiwa majaribio Japan… pichaz na video.

nissan 3Taarifa ikufikie kutoka Samukawa, Kanagawa Japan ambako stori kwenye headlines ni kampuni ya Nissan kupata furaha kubwa baada ya kufanikiwa kwa jaribio la gari walilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe.
Unaambiwa limetembea umbali wa kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya aina mbalimbali barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za barabarani, taa za kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka barabara.YMo_system_rear_0826Nissan wamesema wanalengo la kuanza kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa, hiyo itakua mwaka 2020 ambapo gari hili lina kamera maalum pamoja na sensors zinazofanikisha kulipa taarifa ya tukio husika kwa wakati huo ndio maana linaweza kufanya kama inavyotakiwa mfano kushika breki, kukanyaga mafuta na vitu vingine.
Kingine cha kushangaza, kwa mfano kwenye miji mikubwa ambayo parking ni tatizo unaweza kuliacha likajiendesha lenyewe kwenda kutafuta parking wakati wewe unawahi mahali alafu ukimaliza shughuli zako unalikuta linakusubiri likiwa limepaki vizuri kabisa.nissan 4 
Baada ya kutazama hizo picha hapo juu, unaweza kutazama hii video kujiridhisha kikamilifu aisee japo hii video sio ya majaribio yaliyofanyika saa kadhaa zilizopita..
Tanzanianewz.blogspot.com 

Kurasa za mwazo na mwisho magazetini leo November 27 2013



Kurasa za mwazo na mwisho magazetini leo November 27 2013

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Jumanne, 26 Novemba 2013

Habari za Vijana mwanzo wa Mahusiano na Mapenzi Mapenzi na Ujana hasaya Utotoni hatari sana!Tazama vijana wengi tunavyoweza kupoteza ndoto zetu kisa Kulazimisha mapenzi

 Habari za Vijana mwanzo wa Mahusiano na Mapenzi
Mapenzi na Ujana hasaya Utotoni  hatari  sana!Tazama vijana wengi tunavyoweza kupoteza ndoto zetu kisa Kulazimisha  mapenzi

 Tanzanianewz.blogspot.com




Mwanzoni sikumpenda kutoka
moyoni, nilimpenda kwa kuwa tyu
alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi
nilimtamani tu….yaani nilitegemewa
akinivulia nguo zake tukashiriki
tendo hamu yangu itaisha na
nitaachana naye.
Alinipenda sana, kadri siku
zilivyokwenda alizidisha upendo
wake kwangu.
Hakuna nilichohitaji kwake
akaninyima, aliwahi kumdanganya
baba yake kuwa anaumwa
akatumiwa pesa ilimradi anipatie
mimi nilipomwambia kuwa kuna
mtu ananidai.
Haikuwa kweli pesa ile niliitumia
kulipia chumba nikafanya uzinzi na
Fatuma.
Alihadithiwa habari hiyo, akalia kwa
uchungu mbele yangu, lakini neno
lake la mwisho likabaki kuwa
‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI
MWANAUME WA MAISHA
YANGU’……..Nilijisikia vibaya lakini
nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa
nilimkuwa katika mahusiano na
msichana yule kwa sababu moja tu…
NGONO…na katu hakutaka kushiriki
ngono na mimi. Alinikwepa sana
hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi
huenda ana mtu mwingine.
Msichana mrembo kama huyo
kamwe asingeweza kuishi bila
kufanya mapenzi. Hakika
haikuniingia akilini.
Nikaendelea na vimbwanga vya hapa
na pale.
Hakuchoka kunibembeleza,
hakuchoka kunipenda.
“Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa
nilikuwa nakupenda..” aliwahi
kunambia neno hilo. Japo lilinigusa
lakini sikulitilia maanani.
Hatimaye tukamaliza shule,
nikategemea kuwa ule muda wa
kumfaidi msichana yule kingono
ulikuwa umewadia.
Lakini haikuwa hivyo, akaendelea
kuwa mgumu huku akijitetea kwa
sabab u zisizokuwa na kichwa wala
miguu.
Sasa nikajikuta katika pepo mbaya,
nikaanza kumwonyesha hadharani
kuwa nina wanawake wengine. Japo
chozi lake liliniumiza sana lakini
sikujali.
Kwa nini ananinyima penzi binti
huyu? Nilijiuliza.
Hatimaye nikafikia uamuzi wa
kuachana naye.
Lakini siwezi kuachana naye bila
kumjua ladha yake.
Nikampangia shambulizi moja la
mwisho na kama ni ubaya uwe
ubaya tu.
Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa
mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai
hapa na pale nikamgusa matiti yake
madogo yaliyosimama wima
yakijitahidi kunidhihaki.
Nikamgusa huku na kule..nilipotaka
kumvua nguo akanizuia.
Nilikuwa nimelewa, nikaamua
kutumia nguvu, niliamua
KUMBAKA…..nikaichana sidiria yake,
kisha nikaiondoa chupi yake sasa
akabaki yu uchi wa mnyama.
Nikamrukia ili niweze kutimiza
lengo…
Kamwe sikuwahi kumwona binti
huyu akiwa katika uoga namna ile…
alikuwa amekodoa macho yake….na
alikuwa anatetemeka…
Akataka kukimbia uchi, nikamdaka
mkono.
Mara akatokwa na kelele kubwa sana
zilizonishtua sana.
Amakweli sikuzitegemea.
“ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI
ANANIBAAAKA…..”
Kelele zikawafikia wasamalia wema,
binti akaendelea kupiga kelele.
Hatimaye mlango ukavunjwa,
wasamaria wakanivagaa na kuanza
kunipiga……nilipigwa nikapoteza
fahamu.
Nilipozinduka nilijikuta na pingu
mkononi, pingu iliyounganishwa na
kitanda.
Nilikuwa na maumivu makali mwili
mzima. Nikakumbuka kuwa
nilifumaniwa nikitaka kufanya
ubakaji.
Baada ya kujitambua nilirejeshwa
mahabusu.
SIKU NNE baadaye nilikuja
kutolewa……hapakuwa na dhamana
lakini ilikuwa barua tu ya
kustaajabisha niliyokutana nayo.
“Mpenzi Christopher…..haikuwa nia
yangu kukusababishia kipigo kikali
na kuitwa mbakaji…nimefanya haya
kwa sababu nakupenda…napenda
uishi miaka mingi..Chriss ni wewe
mwanaume pekee niliyetokea
kuvutiwa naye kihisia…lakini nina
mapungufu makubwa…nina kasoro
kubwa…..Chriss mimi ningekuwa
muuaji iwapo ningekuruhusu
unibake….hivi chriss unadhani
mpapaso wako haukunisisimua?
Nilisisimka haswa na nilitamani
nikutimizie kwa hiari lakini
nisingeweza kukuua, ….Chriss ninayo
furaha na wala usisikitike kusikia
hili, mimi nimefurahi sana kufa
nikiupigania uhai wa mwanaume
niliyempenda, ninayempenda na
ninayekufa kwa ajili yake. Kitanzi
hiki kiwe kumbukumbu yako milele
kuwa NILIKUPENDA…….Chriss mimi
ni muathirika wa gonjwa la
UKIMWI…..laiti kama ungenibaka
basi leo hii ningekufa nikiwa
MUUAJI…ninafurahi kuwa nakufa
kama SHUJAA.”
Nilijikuta napoteza fahamu tena,
nilipozinduka nilikuwa nyumbani
kwetu…kila jicho lilinitazama kwa
namna yake……
AMA KWA HAKIKA nilikuwa na
mpenzi aliyenipenda kwa dhati…….
UPUMZIKE PEMA PEPONI…..kamwe
sitakusahau

Picha za mkesha wa Kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Sharo Milionea afariki dunia

 Tanzanianewz.blogspot.com

Picha za mkesha wa Kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Sharo Milionea afariki dunia

DSC01943
Ilikua ni mwezi November tarehe 26 2012 majira ya sa 2 usiku ndipo ziliposambaa taarifa za kifo cha mwigizaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ Hussein Ramadhan Mkieti ‘SHARO MILIONEA’
Leo tarehe 26 november 2013 familia inafanya kisomo kwa ajili ya kumkumbuku ya Sharo milionea huku nyumbani kwao Lusanga-Muheza,Tanga  ambapo hiyo picha ya kwanza wanafunzi wa madrasa wakiimba kaswida kwenye mkesha huu wa kumuombea marehemu Sharo Milionea
Jana tarehe 25 November kulikua na mkesha maalum ulioambatana na kaswida mbalimbali zinazoimbwa na Wanafunzi wa madrasa, Miongoni mwa watu waliohudhuria kisomo hiki ni pamoja na Kitale ambae alikua rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea.
DSC01971
millardayo.com imepiga exclusive interview na mama mzazi wa sharomilionea pamoja kitale juu ya kazi zilizoachwa na marehemu Sharo Milionea ikiwemo mikataba mbali mbali na makampuni kama ya airtel,azam pamoja na movie ambazo aliziacha marehemu sharo.
DSC01901
‘Dhumuni la mkesha huu ni kumkumbuka mwanangu,kwa kutaka kumsomea dua ili mwenyezi Mungu ampunguzie mazito na kumpunguzia madhambi yake,Mpaka sasa mtandao wa Airtel peke ake ndo walinipatia pesa ambapo walinipa jumla ya milion 10,lakini wengine kama Azam wao walikuja kutoa rambi rambi zao nikasikia kule wamefuta mkataba’.
‘Nimefatilia juu ya kiwanja chake kilichokua bunju alichotafutiwa na mjomba wake,nikamwambia mjomba wake akiuze  kwa sababu ya usumbufu maana mi nipo mbali huku,maana nilikua kila siku nasikia mara wamekichota’.
gariii
‘Kuhusu Gari ya Marehemu alikua nayo mudy suma ambaye ni rafiki wa marehemu kwa hiyo mudy suma nilimwambia aliuze lile gari,na kweli mudy suma kaliuza lile gari na pesa akaniletea.
‘Kwa hiyo bado movie tu ndo ninayoijua katika vitu walivyonambia rafiki zake kuwa marehemu alikua na hiki na hiki ni pamoja na movie kwa hiyo movie bado ndo sijapata hela,nimeambiwa ni movie moja ambayo amecheza yeye na kitale na mudy suma’.Mama sharo
DSC01892
DSC01943
DSC01939

Magazeti ya leo November 26 2013 ya Udaku, Michezo na Hardnews

 Magazeti yako leo Nov 26 

Magazeti ya leo November 26 2013 ya Udaku, Michezo na Hardnews

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.